Belle 9 asema hapendi kiki kama wasanii wengine

0
503

Mwanamuziki wa Bongo fleva, Belle 9 amesema kuwa anaamini kazi yake ni kubwa zaidi ya kiki zilizozoeleka kutafutwa na wasanii.

Belle 9 amesema muziki wake una nguvu tofauti na kiki ambazo zimezoeleka hapa mjini kutoka kwa wasanii mbalimbali wanavyo tumia mapenzi, skendo, familia ili wajulikane au wazungumziwe.

Mwanamuziki huyo amesema muziki wake ni mkubwa kuliko kiki ambazo zinaendelea hapa mjini huku akitolea mfano kwamba hawezi kuonesha familia yake kwa kuwa yale ni maisha yake binafsi na familia yake na hawezi kuweka kwenye mitandao.

Belle 9 amesema kuwa kama mtu anataka kutafuta ‘kiki’ kuhusu yeye basi itamlazimu aishi karibu naye sana au na familia yake ili kutengeneza ‘kiki’ japokuwa bado itakuwa ni ngumu kutokana na mfumo wa maisha anaoishi kwa kuwa hapendi kuzungumziwa mbali na muziki.

mwanamuziki huyo kwasasa anaishi mkoani Dar es Salaam kwa ajili ya kupata urahisi wa kufanya kazi zake za muziki akitokea Morogoro.

Bele 9 siku mbili nyumba aliwashangaza watu baada ya kusema kwamba albamu yake ijayo itavunja rekodi ya Michael Jackson na Bob Marley, swali la kujiuliza kama kasema hatafuti kiki sasa hizo siyo kiki?.

LEAVE A REPLY