Belle 9 afunguka video yake inayosambaa mitandaoni akiwa na mwanamke mbali na mkewe

0
335

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Belle 9 amefunguka video ambayo ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha akiwa na mwanamke mwingine mbali na mama watoto wake.

Watu wengi hawajamzoea Belle 9 kuwa aina ya msanii ambaye anapenda kiki kwaiyo kitendo cha video iliyomuonyesha mwanamuziki akiwa na mwanamke mwingine katika pozi la kimahaba kuashiria kabisa wana uhusiano wa kimapenzi liliwashtua watu wengi.

Inafahamika kuwa Belle 9 anaishi na familia yake na kwa sasa ana watoto watatu na anaishi na mama watoto wake sasa video ike  iliposambaa akiwa na mwanamke mwingine ambaye anasemekana ni mchepuko wake ilisababisha minong’ono mikali mtandaoni.

Belle 9 amekataa amekanusha taarifa hiyo kuwa mrembo yule ni mchepuko wake bali alidai kuwa ile video ni ya zamani ila aliwahi kuwa mpenzi wake hapo nyuma.

LEAVE A REPLY