Belle 9 achagui wakufanya nae kazi

0
33

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Belle 9 amefunguka na kuweka wazi kuwa katika utaratibu wake wa kufanya kazi haangalii wala kuchagua wa kufanya naye kazi.

Belle 9 amesema kuwa “Najua watu huwa tunasahau fadhila na mimi kiukweli nisiwe mchoyo wa kutoa shukurani, ninamshukuru sana, Ben Pol kwa mambo aliyoweza kunifanyia mpaka hapa nilipofikia.

“Alikuwa mwalimu mzuri sana kwangu na alikuwa anapenda nitimize ndoto zangu, hakutaka nikate tamaa kabisa,” anasema Darasa.

Pia msanii huyo amesema kuwa anayejiamini kwenye kazi zake haoni sababu ya kuanza kuchagua watu wa kufanya nao kazi, bali kuona wasanii wachanga wanafika mbali.

Amesema “Unajua mimi ni msanii, nipo kwenye gemu na ninaulewa muziki vizuri, ukiwa msani unatakiwa usichague kazi, kwa upande wangu akija msanii yeyote awe mchanga kwenye gemu au mkongwe, napiga kazi, sioni sababu ya kuchagua gereza kama mimi ni mfungwa,”.

LEAVE A REPLY