Bella nae amekuwa ‘team Kiba’?

0
728

Ingawa ni jambo ambalo mashabiki wengi wa muziki hawapendi kulisikia kutoka kwa wasanii wao lakini ukweli unabaki pale pale kuwa kila msanii ana hulka yake.

Baada ya Ali Kiba kuweka wazi kuwa ‘collabo’ sio sehemu ya mkakati wake wa kufanikiwa kimuziki staa mwingine wa Bongo, Christian Bella nae ameweka wazi kuwa ‘HANA MPANGO NA COLLABO’.

Staa huyo anayejiita ‘King of Melodies’ amedai kuwa collabo zinawafanya wasanii wazoeleke kwa mashabiki hivyo kupoteza mvuto ndani ya muda mfupi.

Hata hivyo Bella amebainisha kuwa atakuwa anafanya collabo lakini zitakuwa chache ni atafanya collabo zenye faida kwa muziki wake lakini sio kufanya collabo ili aonekane kuwa nae amefanya collabo.

Je, Bella na Ali Kiba wanaona nini katika hili? Je, hawa ni ‘team moja?’

LEAVE A REPLY