Bella awaponda wasanii wanaotembea na walinzi

0
44

Mwanamuziki wa muziki wa Dansi nchini, Christian Bella amefunguka na kusema kuwa wasanii kutembea na walinzi wengi ni ushamba kwani yeye hawezi kufanya hivyo.

Msanii Christian Bella amewachana wasanii wanaotembea na ulinzi ‘bodyguards’ kwa sababu anaona wamekuwa wengi kuliko wasanii wenyewe wanapokutana kwenye sehemu za show.

Christian Bella amesema mtu hawezi kuwa na Bodyguard watano au sita wakati  nyumbani kwake anapoishi anadaiwa kodi, kitendo hicho ni kukosa fikra katika tasnia ya sanaa ya muziki.

Amesema kuwa “Mimi nimewahi kwenda kwenye show nikashangaa ‘backstage’ kila msanii ana ‘bodyguards’ na wengine wakakomoa wakaja na walinzi sita.

 Pia amesema kuwa “Cha kushangaza walinzi walikuwa wengi kuliko wasanii mpaka nikauliza hawa ndiyo wasanii au basi nilijikuta nacheka sana”.

Ameongeza kusema kuwa “Huwezi kuwa na walinzi wengi huku unadaiwa kodi ingawa siwezi kukasirika nikimuona mtu ana bodyguard wengi ila sio kujibrand ukiwa na walinzi wengi, lifestyle na pesa ndiyo humbeba mtu sio bodyguard kwa mtazamo wangu”.

LEAVE A REPLY