Bella awachana wasanii wenzake kuhusu Ommy Dimpoz

0
133

Mwanamuziki wa Dansi nchini, Christian Bella amefunguka na kusema kuwa amesikitishwa na baadhi ya wasanii kuwasapoti watu wanafariki.

Bella amezungumza hayo baada Ommy Dimpoz, ambaye hivi karibuni alirejea nchini akitokea Ujerumani alikokuwa akitibiwa ugonjwa wa koo uliyokuwa ukimsumbua kwa muda mrefu.

Bella amesema alikuwepo wakati Dimpoz anaanza kuugua koo mpaka kufikia hatua ya kufanyiwa Upasuaji lakini amewalipua watu ambao walimposti Dimpoz wakati akiwa hoi kitandani na kumtakia apone haraka lakini alivyopona hawakufanya hivyo wala hawakuposti wimbo wake mpya aliouachia hivi karibuni.

“Watu walikuwa na wasiwasi sana huenda chochote kikatokea kwa Dimpoz, walimposti sana wakimuombea apone, hadi wale ambao alikuwa haelewani nao walimposti. Baada ya hapo ikafika Birthday yake lakini hao watu hawakumposti, na hata juzi alivyotoa wimbo wake hawakumposti lakini angefariki wangemposti sana’.

Aidha, msanii huyo amemuombea Bella awezekupona kabisa na sauti yake irejee katika hali yake ya kawaida ili aendelee na kazi yake ya sanaa.

LEAVE A REPLY