Bella atangaza kuachia albam mpya

0
23

Msanii wa muziki wa Dansi nchini, Christian Bella ametangaza ujio wa albamu yake mpya itakayotoka mwaka huu baada ya kukamilika.

Bella ambaye ana asili ya nchini DR Congo amesema kuwa kila siku ataachia video ya wimbo mpya mpaka siku ya uzinduzi.

Katika hatua nyingine amesema licha ya ukimya wake, yeye ni msanii kati ya wasanii watatu wa Tanzania ambao wanakubalika na kufanya shoo nyingi na kwamba ataachia video moja kila siku kwa siku tano mfululizo.

Kwa upande mwingine Bella amezungumzia ghorofa zake mbili ambazo amezijenga huko Mbweni jijini Dar es Salaam.

Bella amesema kuwa baada ya kupost clips ya mjengo huo, kuna watu wengi wanamwuuliza kwa nini anamiliki nyumba Tanzania wakati yeye ni raia wa Congo.

Bella amewataka mashabiki wake kujitokeza kwa wingi siku ya uzinduzi wa albam yake kwani amewaandalia mambo makubwa na mazuri.

LEAVE A REPLY