Bella aonyesha mjengo mpya

0
38

Mwanamuzisanii wa muziki wa Dance, Christian Bella ameonyesha nyumba kubwa ya kifahari analomiliki hapa nchini maeneo ya Mbweni jijini Dar es Salaam.

Bella amesema kuwa kiwanja cha nyumba hii alinunua mwaka 2016 na alinunua kwa Tsh Milion 55 kutoka Milion 80 ambayo alikua akihitaji mwenye eneo. Msingi wa Nyumba hii peke yake amesema umegharimu zaidi ya Tsh Milion Mia Moja.

Mwanamuziki huyo ameendelea kusema kuwa Ghorofa hiyo ipo kwenye hatua ya mwisho kukamilika na baada ya muda si mrefu itakuwa imekamilika.

Bella ameedelea kusema kuwa nyumba zote hizi za Bella ziko location moja ambayo ni MBWENI, na ziko hatua chache kutoka Ndege Beach Mbweni, Mwaka huu amepanga kuhamia.

Pia amesema kuwa ujenzi wa nyumba zote hizi mbili zilizopo Tanzania na zingine Mbili zilizopo Kwao Kinshasa (Congo) Pesa zake zimetokana na Muziki wake.

6. Ujenzi wa Nyumba hizi ulianza baada ya kukutana na Ruge Mutahaba baada ya Ruge kumtengenezea thamani ya kulipwa Milion 10 kwa show fedha ambazo hakuwahi kulipwa kabla na hii ilikua 2013.

LEAVE A REPLY