Bella afunguka kuhusu kubebwa na media

0
130

Mwanamuziki wa Dansi, Christian Bella amesema kuwa yeye hawezi kumfikia Muumin Mwinjuma kwa kuwa kamzidi kwa kila kitu na kamwe hawezi kushindana nae.

Kauli hiyo ya Bella imekuja mara baada ya Muumini kudai kuwa Bella anabebwa sana na Kituo cha Radio kwa maslahi yao binafsi.

“Kuhusu ishu ya kubebwa, si kweli bali ni ubora wa kazi zangu ndio unaofanya niwe juu kiasi cha wengine kuamini kuwa nabebwa.

“Nimetoka kwetu Congo kuja Tanzania kwaajili ya kutafuta pesa kupitia muziki. Najitahidi kulisoma soko kila siku na kubadilika kadri ya mahitaji ya soko yalivyo’’.

Bella ameongeza kwa kusema kuwa Muumin ni mkali na anakubalika zaidi kama anavyoamini, na kumuomba atumie ukocha na ugwiji wake kuipandisha juu bendi yake na muziki wa dansi kwa ujumla.

LEAVE A REPLY