Beki wa PSG amekuwa beki wa kwanza kushinda ‘hat trick’ UEFA

0
114

Beki wa kushoto wa PSG, Layvin Kurzawa amekuwa beki wa kwanza kushinda hat trick kwenye mechuano ya klabu bingwa Ulaya.

Beki huyo ameshinda goli hizo wakati timu yake yake ikiifunga Anderlecht bao 5-0 na kuweza kufuzu hatua ya 16 bora.

Kurzawa alikuwa amefunga mabao 17 pekee kabla ya mechi hiyo kuanza lakini akafunga mabao matatu katika kipindi cha pili.

Neymar na Marco Verratti pia walifunga bao kila mmoja wao huku PSG ikifuzu kwa urahisi katika timu 16.

Kurzawa alionyesha ishara za mshambuliaji katika mabao yake mawili ya kwanza akifunga baada ya mpira kugonga mwamba na kurudi uwanjani na baadaye kufunga bao la pili kwa kichwa kabla kufunga bao lake la tatu katikati ya wachezaji wengi.

LEAVE A REPLY