Beka Flavour amtaka Aslay kuachana na kiki

0
1275

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Beka Flavour amefunguka na kumtaka mwanamuziki mwenzake Aslay kuongeza nguvu na maarifa kwenye muziki wake ili aweze kufika mbali zaidi huku akimsii kuachana na masuala ya kiki za mitandoni.

Beka ametoa kauli hiyo baada ya kupita siku kadhaa tokea Aslay kuachana na mama watoto wake na kuamua kuweka wazi ‘penzi’ lake jipya mitandaoni jambo ambalo wengi wameliona kama ni ‘kiki’ ili kusudi aendelee kuzungumziwa midomoni mwa watu.

 Kuna watu wakifanya ‘kiki’ ina wasaidia na muziki wao unaenda inawezekana Aslay ndiyo miongoni mwa hao lakini mimi sijui, ila ninachomshauri afanye muziki mzuri, najua ni mwanamuziki mkubwa ila siwezi kumwambia aache kufanya kiki kwenye mitandao za ku-post mpenzi wake mpya itakuwa haileti maana kwa kuwa mimi sio mzazi wake”,.

Pamoja na hayo, Beka ameendelea kwa kusema “watanzania wamekaririshwa kuwa ili mtu aonekane amefanya muziki mzuri na kuwa maarufu zaidi ya wengine basi lazima utengeneze kiki ya mahusiano ya kutembea na staa mkubwa aidha bongo movie au bongo fleva. Ila kwa katika nafsi yangu mimi siwezi kuliamini hili”.

LEAVE A REPLY