Beka Flavour akanusha kuwa chanzo cha kuvunjika Yamoto Band

0
110

Msanii wa Bongo Fleva, Beka flavour amefunguka na kusema kuwa yeye siyo sababu ya kuvunjika kwa Yamoto Band bali kila mmoja aliamua kufanya kazi kivyake.

Beka amesema kuwa mashabiki inatakiwakufika sehemu na kukubaliana na matokeo na  kuwa kila kitu kina muda wake lakini sio kurusha lawama na kumtafuta mchawi nani katika hilo, Hata hivyo swala la kuvunjika kwa kundilimeweza kusababisha watu kujiongeza na kupambana zaidi.

Pia Beka amesema kuwa kwa kumbukumbu yake anajua kabisa kuwa hakuwahi kugombana na mtu katika lile kundi zaidi ya mmoja tu na haikusababisha kugombana sana kwa sababu walikuja wakakaa sawa.

Wasanii hawa walikuwa wakifanya kazi pamoja katika kundi moja lakini baadae kila mmoja alikwenda na njia yake baada ya kundi hilo kushindwa kuendelea.

Wasanii waliokuwa wanaunda kundi hilo ni Aslay ambaye anafanya kazi kivyake chini ya King Empire, Beka Flavour ambaye pia anafanya kazi kivyake, Enock Bella nae anafanya kazi kivyake pamoja na Marombosso ambaye yupo WCB.

LEAVE A REPLY