Beka Flavour afunguka kuachana na mpenzi wake

0
345

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Beka Flavour ametangaza kuachana na mama watoto wake kwa sababu ya watu kufuatilia sana mahusiano yao.

Beka amesema kuna watu kazi yao ni kufuatilia maisha ya watu maarufu na wanapogundua hutaka kuanzisha stori.

“Ni kweli hatupo pamoja kwa sasa, sijafuata mkondo wa Aslay, watu wengi wameachana na mahusiano yao mengi tumeyafahamu kupitia mitandao ya kijamii.

Pia amesema kuwa mahusiano mengi yapo mengi ambayo hatuyafahamu hawajayaweka mitandaoni, hata mimi kwangu sikutaka watu wajue kama nimeachana na mama watoto wangu” amesema Beka Flavour.

“Unajua sasa hivi kuna wambea, udaku na ufukunyuku mwingi na watu wapo kwa ajili ya kazi hiyo ni kufuatilia maisha ya watu maarufu, wakigundua wanataka kutengeneza stori na walijaribu kufanya hivyo japokuwa mimi sikuliweka hadharani ila sasa hivi limenifikia” ameongeza.

Beka Flavour na mpenzi wake huyo wamejaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume aitwaye Aaryani ambaye ana umri wa mwaka mmoja na miezi minne.

LEAVE A REPLY