Beka Flavour adai hana mpango wa kuachia albam

0
85

Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Beka Flavour amesema kuwa kwasasa hafikirii kuachia albamu kutokana na soko la albamu kushuka nchini.

Beka Flavour ambaye alikuwa anaunda kundi la Yamoto Band amesema kuwa kwasasa amejikita katika vitu vingine ambavyo anaona vitamuingizia fedha kwa urahisi kupitia muziki wake kuliko kuwaza kutoa albamu.

Pia msanii huyo amesema kuwa albam ni kitu ambacho kipo lakini kwasasa anakiweka pembeni kwa sababu hana uwezo wa kutoa albamu.

Beka ameendelea kusema kuwa  mauzo ya albamu magumu sana sasa hivi tofauti na kipindi cha nyuma ambacho wasanii walikuwa wanatengea mauzo ya albamu kuliko njia nyingine.

Wasanii wengi nchini kwasasa hawapendi kuachia albamu kutokana na soko kushuka nchini hivyo kila mmoja anategemea kuuza nyimbo zake kwenye mitandao kama vile Youtube, Mdundo.com pamoja na wasafi.com.

LEAVE A REPLY