Beka Flavor akunusha kufunga ndoa kimya kimya

0
100

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Beka Flavor amekanusha taarifa za kufunga ndoa kimya kimya kama inavyosambazwa katika mitandao ya kijamii.

Beka Flavor alishawahi kusikika akisema kuwa hawezi kumuanika mpenzi wake Kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu hajatoa mahari kwao.

Lakini baadae alianza kumuanika mitandaoni na hata kuonekana ni mjamzito na baadae ilisemekana wawili hao wanaishi nyumba moja na Habari za chini ya kapeti zikadai wawili hao wamefunguka ndoa kwani Msichana huyo alibadilisha dini.

Beka Flavor amefunguka na kusema hawezi kuanika kila kitu kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwa ana maisha yake mbali na mziki hivyo hawezi kuweka maisha yake katika mitandao ya kijamii.

Pia mwanamuziki huyo amethibitisha ameshamvhumbi mpenzi wake huyo na hivi sasa muda wowote wanategemea kuzaa mtoto wao wa kwanza.

LEAVE A REPLY