Bei ya petroli na dizeli yaongezeka

0
116

Mamlaka ya udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA),imetangaza bei kikomo za mafuta kwa mwezi huu huku petroli na dizeli zikiongezeka.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Nzinyangwa Mchany amesema bei hizo zitaanza kutumika leo ambapo amesema bei za jumla na rejareja za mafuta yote yaliyoingizwa nchini kupitia bandari ya Dar es Salaam zimeongezeka ukilinganisha toleo lililopita.

Mchany amesema kuwa mwezi huu bei za reja reja za petroli zimeongozeka kwa shilingi moja kwa lita ikiwa ni sawa na asilimia 0.06 na dizeli kwa shilingi 69 kwa lita sawa na asilimia 3.37 na mafuta ya taa shilingi nne kwa lita sawa na asilimia 0.20.

Kaimu Mkurugenzi hyo amesema kuwa kwa kiasi kikubwa ongezeko la bei za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa kwenye soko la ndani limetokana na mabadiliko ya bei za m afutas katika soko la Dunia na kuongezxeka na gharama za usafirishaji w mafuta pamoja na kushuka kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola ya marekani

Mamlaka ya udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA),imetangaza bei kikomo za mafuta kwa mwezi huu huku petroli na dizeli zikiongezeka.

LEAVE A REPLY