Beckham azindua timu yake nchini Marekani

0
444

Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Uingereza na klabu ya Manchester United, David Beckham amezindua timu yake ya soka huko Miami nchini Marekani.

Beckham alichungulia fursa hiyo katika harakati za kufunga mkataba timu yake ya zamani ya LA Galaxy mwaka 2014.

Timu hiyo haijatajwa mpaka sasa ingawa inatarajiwa kucheza mbele ya umati wa watu elfu ishirini na tano mjini Overtown na katika viwanja vilivyoko karibu na mji huo.

Baada ya uzinduzi huo David Bekham alipongezwa na watoto wake wanne kwa njia ya video maalum akiwemo mkewe Victoria, ambaye aliwahi kuwa mwanamuziki wa zamani wa kundi la Spice Girl , mshindi mara 23 wa michuano ya Grand Slam Serena Williams, mshindi mara nane wa medali ya dhahabu wa michuano ya Olimpic Usain Bolt na watu wengine maarufu akiwemo Brady, Will Smith, Jay Z na Jennifer Lopez.

Beckham, alijiunga na timua ya LA Galaxy akitokea timu ya Real Madrid mnamo mwaka 2007, na kuwa mchezaji wa kwanza mstaafu kumiliki timu katika ligi.

Niliamua kuondoka Real Madrid na kwenda kwenye ligi ambayo ilikua inasuasua, ilikuwa ni hatua kubwa mno niliyopiga na kitu kimoja ninachokijua ni kuwa hatua hiyo itazaa matunda yenye changamoto lakini changamoto zenye kusisimua.

Uzinduzi huu haikuwa kazi rahisi kwa muda wa miaka minne ya utafutaji kiwanja eneo la kusini mwa Florida huku tukipingwa na baadhi ya watu katika maeneo kadhaa.

Washirika wa David Beckham walinunua ardhi tayari kwa kujenga uwanja wao mnamo mwishoni mwa mwaka 2015, baada ya kushindwa mara tatu kununua eneo walilolitaka na bora zaidi kwa shughuli hiyo.

LEAVE A REPLY