Batuli awataka waigizaji wenzake wawe na ushirikiano

0
224

Muigizaji wa Bongo Movie, Yobnesh Yusuph maarufu kama ‘Batuli’ amewataka mastaa mbalimbali kujenga utamaduni wa kupendana na si kuchukiana kama ilivyo kwa baadhi yao.

Msanii huyo aliyasema hayo baada ya kuona baadhi ya wasanii wakiwa pamoja katika msiba wa aliyekuwa mpendezeshaji wa video nchini, Agness Gerald maarufu kwa jina la Masogange.

“Giza aliwezi kuondoa giza bali mwanga pekee ndio wenye nguvu ya kuondoa giza, chuki haiwezi kuondoa chuki bali upendo tu ndio wenye nguvu kubwa ya kuondoa chuki.

“Wasanii huu si wakati wa majungu, maisha ni mafupi sana tunatakiwa kupendana na si chuki katika kazi au mafanikio ya mtu,” alisema Batuli.

LEAVE A REPLY