Batuli afungukia afya yake

0
195

Muigizaji nyota wa Bongo Movies Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ amesema kwa sasa yuko fiti tofauti na watu walivyokuwa wakisema ana hali mbaya.

Batuli amesema amegundua watu wanapenda kuona mtu anapata matatizo kisha kufurahia, lakini Mungu amesimama na yeye na sasa yupo okee kabisa.

“Mungu halali, ukweli ni kwamba alikuwa macho kwangu na hata sasa ananipigania. Sasa hivi niko fiti kabisa, namuomba Mungu azidi kunipa afya njema ili adui zangu waumbuke,”.

Amesema Batuli ambaye aliibua taharuki kiasi cha baadhi ya kurasa za udaku mitandaoni kuzusha amekufa.

LEAVE A REPLY