Bastian Schweinsteiger ‘out’ Old Trafford

0
106

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ameanza kukunjua makucha yake kwenye kikosi cha United baada ya kuwaambia wachezaji 9 wa kikosi hicho kutafuta timu za kwenda kuchezea.

Miongoni mwa majina ya wachezaji hao lipo jina kubwa moja la nahodha wa timu ya taifa ya Ujerumani na mshindi wa medali ya kombe la dunia, Bastian Schweinsteiger.

Kwenye mazoezi ya jana ya kikosi cha kwanza cha United, Mourinho hakuwajumuisha wachezaji kadhaa akiwemo Bastian na inadaiwa kuwa alikuwa na kikao na kila mmoja wao kwaajili ya kuwaeleza kuwa hawana nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha United kwa msimu huu.

Wachezaji waliokosekana kwenye mazoezi ya kikosi cha kwanza siku ya jana pamoja na Schweinsteiger ni Adnan Januzaj, Cameron Borthwick-Jackson, Tim Fosu-Mensah, Andreas Pereira, Will Keane, Tyler Blackett, Paddy McNair na James Wilson.

Katika hatua nyingine, kwa mara ya kwanza siku ya jana mashabiki wa Manchester waliweza kumuona mshambuliaji wao mpya, Zlatan Ibrahimovich akiichezea timu hiyo baada ya kumaliza likizo na kuanza mazoezi na wenzake.

Manchester United ilimnunua Bastian Schweinsteiger kwa £6.5million miezi 12 iliyopita wakati wa uongozi wa Louis van Gaal.

LEAVE A REPLY