BASATA wazifagilia ‘EATV Awards’

0
148

Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limekipongeza kituo cha East Africa Television kwa kuanzisha tuzo kubwa za wasanii wa muziki na filamu kwa Afrika Mashariki.

 

Ofisa Habari wa BASATA Bw. Aristides Kwizela amesema kitendo hicho ni kitu kizuri kwani kinaonesha kuthamini mchango wa kazi za sanaa pamoja na wasanii wenyewe.

 

Kwizela amesema kwa niaba ya BASATA na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo linawapongeza sana East Africa Television kwa sababu ni kituo cha kwanza ambacho kimeona kuna haja ya kuja na tuzo ambazo kwa kweli ni kuthamini mchango wa wasanii.

 

Pamoja na hayo BASATA wamewataka wasanii kufanya kazi zenye ubora zaidi ili ziweze kuwa na viwango vizuri kwenye ushindani wa tuzo hizo pamoja na soko la kimataifa.

LEAVE A REPLY