BASATA wampongeza AT baada ya kushinda tuzo mbili

0
138

Baraza la sanaa la Taifa (Basata) limempongeza mwanamuziki wa Bongo Fleva, AT baada ya kushinda tuzo mbili za Mama Awards nchini Marekani.

AT alishinda tuzo hizo katika vipengele viwili tofauti yaani  International Artist na Best  Music Video.

BASATA waliposti video hizo katika ukurasa wao wa instagram na kuandika salamu za pongezi hizo kwa mwanamuziki huyo.

Basata wameandika kama ifuatavyo kwenye ukurasa wao wa Instagram

Mwanamuziki  maarufu katika miondoko ya mduara  nchini Ally Ramadhani, kwa jina la kisanii kama AT, ameshinda tuzo mbili za MAMA AWARDS huko nchini Marekani. Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kama mlezi wa wasanii nchini  linampongeza kwa dhati msanii AT  kwa heshima na  sifa kubwa walioipatia Taifa, huko ughaibuni. Aidha BARAZA linapenda kuchukua nafasi hii  kuwasihi wasanii wengine nchini  kuongeza ubunifu na ubora zaidi  kwenye kazi zao ili sanaa yetu iweze kufika mbali  zaidi kimataifa.

Mwanamuziki huyo alishinda tuzo hizo mapema mwezi huu nchini Marekani ambapo pia wanamuziki wenzake Alikiba na Nandy walishinda tuzo za AFRIMA nchini Nigeria.

LEAVE A REPLY