Basata wampa onyo kali Diamond kufanya shoo nchini Kenya

0
302

Baraza la Sanaa nchini (BASATA) limemuonya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kutofanya shoo yoyote nchini Kenya baada ya kufungiwa.

Licha ya meneja wake kuahidi kufanyika kwa shoo katika mji wa Embu nchini Kenya mwisho mwa mwaka huu, Baraza hilo limempa onyo endapo atakiuka atapewa adhabu zaidi ya hapo.

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewafungia Diamond Platnumz na Rayvanny kutofanya shoo yoyote ndani na nje ya Tanzania baada ya kuimba wimbo wa ‘Mwanza’ ambao ulifungiwa na Baraza hili kutokana na kukosa maadili katika jamii.

Pia Baraza hilo limesitisha Tamasha la Wasafi kutokana na kutokidhi vigezo vya uombaji wa ufanyaji shoo ndani ya Baraza hilo.

Diamond na lebo yake ya WCB walikuwa wanatarajia kufanya shoo katika mji wa Embu siku ya Desemba 24 mwaka huu pamoja na Mombasa Desemba 26 mwaka huu.

LEAVE A REPLY