Basata wamfungulia Dudu Baya

0
85

Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limemfungulia Dudu Baya baada ya kusamehewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe.

Baraza hilo limetangaza uamuzi wa kumfungulia leo, Februari 12, 2020 baada ya kumfungia kwa kipindi kisichojulikana tangu mwaka jana kwa kile ilichoeleza kuwa amekiuka maadili kwa maneno aliyoyasema kwenye mitandao ya kijamii.

Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Godfrey Mngereza amesema kuwa Dudu Baya alikata rufaa kwa Waziri Mwakyembe, kama inavyoelekeza Sheria iliyounda Baraza hilo.

Alisema kuwa Waziri alimsikiliza na kumsamehe hivyo kwa mujibu wa sheria hiyo Baraza hilo pia linamtoa kifungoni na kuendelea na muziki kama kawaida.

“Sheria ya Baraza namba 23 ya Mwaka 1984 pamoja na marekebisho yake yaliyofanywa mwaka 2006 inaeleza kuwa mtu yeyote akipewa adhabu na Baraza anaweza kukata rufaa kwa Waziri; na atakachosema Waziri ndicho kitakachotekelezwa,” amesema Mngereza.

LEAVE A REPLY