Barnaba akiri kuachana na mama Steve kulishusha muziki wake

0
99

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Barnaba amefunguka na kukiri kwamba muziki wake ulishuka baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi ambaye amezaa nae mtoto mmoja.

Barnaba amefunguka na kusema kuwa moja ya kitu ambacho kimeua sana muziki wake kwa kipindi kifupi cha nyuma ni kutokana na ugomvi kati yake na mama Steve.

Msanii amesema kuwa mama steve ni mwanamke aliewahi kuchukua sehemu kubwa sana katika maisha yake lakini kwa sasa anaamini kuwa  kila mtu anatakiwa kuendelea na maisha yake baada ya kuachana.

Barnaba alisema kuwa siku zote amekuwa akimpenda na hatokaa kumchukia kabisa mama steve kwa sababu ni mama wa mtoto wake na kla siku wataendelea kuwasiliana kwa sababu wana kitu kinawaunganisha  ambacho ni mtoto.

Barnaba na mama steve waliweza kukaa katika mahusiano kwa zaidi ya miaka 10 pamoja na kufanikiwa kupata mtoto mmoja.

LEAVE A REPLY