Barnaba ahofia kupiga picha na wanawake

0
1510

Mwanamuziki wa Bongo Fleva anayefanya vizuri na kibao chake cha ‘Chausiku’ Barnaba Boy amefunguka na kuweka wazi kuwa hivi sasa anahofia sana kupiga picha na wasichana kwa kuhofia uzushi.

Kuali hiyo ya Barnaba inakuja kufuatia baadhi ya watu kumzushia kuwa anatoka yupo kwenye mahusiano na mwanamke ambaye anapiga naye picha.

Barnaba amefunguka hayo baada ya kuulizwa kuhusu picha zake na wasichana kadhaa ambazo zimekuwa zikionekana Kwenye mitandao ya kijamii na kudaiwa kubadilisha badilisha wasichana.

Barnaba ameweka wazi kuwa wasichana wengine ni mashabiki zake akikutana nao wanaomba picha lakini baadae anasingiziwa ni wanawake wake.

Pia Barnaba alikataa taarifa kuwa tangu ameachana na mama watoto wake Mama Steve amekuwa na wanawake wengi suala ambalo amelipinga vikali.

LEAVE A REPLY