Barnaba afunguka siri ya ubora wa sauti yake

0
153

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Barnaba amefunguka sababu ya sauti yake kuendelea kuwa imara tofauti na wasanii wengine.

Barnaba ambaye ni zao la THT amesema kuwa  kila anapojua kuwa anatarajia kufanya shoo sehemu amekuwa akijitahidi sana kutunza sauti yake ili aweze kufanya vizuri katika  shoo zake.

Ameongeza kwa kusema kuwa amekuwa akifanya mazoezi, amekuwa akijitahidi kupumzika sana na hata kupunguza swala la kufanya mapenzi ili kuweza kumtain nguvu zake.

Pia Barnaba amesema kuwa anazingatia kupumzika muda mwingi na kuwahi kulala sana hili kupumzika kwa sababu show ninayoenda kuifanya ni kubwa sana.

Vile vile ameongeza kwa kusema kuwa anajitahidi kutokula vyakula vya wanga kama mahindi, maharage, mtama maana hivyo ni vyakula vinavyoweza kuacha mabaka kooni na kusababisha sauti kutoka kwa shida na kukuumiza koo.

Kingine anachozingatia amesema kuwa anajitahidi sana kunywa maji mengi na kwa wingi zaidi ya kawaida ili kupata nguvu.

Kitu kikubwa pia nazingatia sana katika kufanya mazoezi ya mwili kama kukimbia na kupiga push-up kwa sababu ya kutafuta pumzi maana kuimba muda mrefu kunahitaji pumzi sana.Lakini katika vyote ninaweza nisifanye mapenzi hii wiki nzima mpaka show ipite.

 

 

LEAVE A REPLY