Barnaba adai kwasasa yupo single

0
214

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Barnaba amesema kuwa kwasasa hayupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwanamke yoyote endapo akiwa kwenye mahusiano watu wafahamu.

Barnaba amefunguka hayo baada ya picha zake kuzagaa  kwenye mitandao ya kijamii na kupelekea baadhi ya watu kudai huwenda wanawake hao anatoka nao kimapenzi nasio vinginevyo.

Amesema kuwa “Sijui chochote kinachoendelea, nilisema siku ambayo nitakuja kumtangaza mwanamke wangu basi kuna mawili naoa au namvisha pete ya uchumba kwa hiyo sina mapenzi ya mitandao.

Pia amesema kuwa mpenzi wake ampendae kwa hawezi kumuweka kwenye mitandao ya kijamii kama walivyo watu wengine.

Barnaba ameendelea kwa kusema “Barnaba tayari ni ‘star’ na watu wakiniona nipo nimesimama na mwanamke huyu mara yule wanahisi labda ni wapenzi wangu.

LEAVE A REPLY