Barnaba na Dulla Makabila kushiriki Sauti za Busara

0
14

Wanamuziki maarufu Bongo, Barnaba na Dulla Makabila wanatarajiwa kushiriki tamasha la sauti za  Busara litakalofanyika visiwani Zanzibar mwezi Februari.

Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Yusuf Mahmoud amesema jumla ya vikundi saba kutoka nje ya nchi na saba wa ndani ya nchi watashiriki wakiwemo wasanii Barnaba na Dulla Makabila.

Hata hivyo amesema tamasha hili kwa mwaka huu likiwa mara yake ya 18 kufanyika lina kauli mbiu ya ‘Mazingira Yetu, Maisha Yetu’ ikiwa ina lengo kuu ya kukuza ufahamu, mazungumzo na hatua za mabadiliko juu ya mabadiliko ya hali ya hewa ambayo tayari yamefikiwa kiwango cha dharura kote ulimwenguni.

Naye Meneja wa tamasha hilo, Journey Ramadhani amesema tofauti na miaka mingine ambapo tamasha hilo hufanyika siku nne kwa mwaka huu litafanyika siku mbili yaani Februari 12 hadi Februari 13, 2021.

Balozi wa Norway nchini, Elizabeth Jocobsen amesema tamasha hilo limekuwa likisaidia kwa kiasi kikubwa kutangaza utamaduni wa Mwafrika na kuongeza kuwa utamuduni kwa wasiojua ni haki na Sera ya maenedeleo kwa watu wake hivyo ipo haja ya kuendelezwa nankuenziwa kila iitwapo leo.

Wakati balozi wa Umoja wa Mataifa, Mantredo Fanti amesema muziki kama hiphop, Rock na blues chanzo chake ni muziki wa Afrika na kueleza kuwa kuwa waafrika wana kila sababu ya kujivunia muziki wao na utamaduni wao.

Vikundi vitakavyoshiriki katika tamasha hilo ni pamoja na nchi vinapotoka kwenye mabano, Yugen Black rock (Afrika Kusini), Moreleraba (Lesotho), Djam (Algeria), Sika Kokoo Kokoo (Ghana), Dawda Jobarten (Gambia), SitiMuharam (Zanzibar), Sandra Nankoma (Uganda), Stone Town Rockerz (Zanzibar), Richie Lumambo (Tanzania) na Dogo Fire (Reunion)

Kiingilio katika tamasha hilo kwa watanzania na watu kutoka nchi za Afrika Mashariki kwa siku zote mbili ni Sh10, 000 wakati kwa siku moja ni Sh6000.

LEAVE A REPLY