Barakah The Prince na Lord Eyez: Tatizo ukongwe au mafanikio kwenye kazi?

0
200
Baraka The Prince

Kuna mengi yamezungumzwa tangu staa wa Rocka4000, Barakah The Prince alipoamua kuweka hadharani kuwa staa wa zamani wa kundi la WEUSI, Lord Eyez atakuwa chini ya kampuni yake.

Taarifa hiyo ilimtoa mafichoni member wa kundi la WEUSI, Bonta ambaye aliponda hatua hiyo na kudai Lord Eyez amejidhalilisha lakini memba mwingine Joh Makini akasema ‘sio ishu mbaya’ ni uamuzi wa mtu na unapaswa kuheshimiwa.

Lakini tatizo ni kuwa wakati Lord Eyez anasota ni kama washkaji zake wa karibu hawakuwa wakijali hususani kumpa nafasi ya kufanya kazi tena leo hii kuna mtu amejitokeza kumsaidia watu wanaponda.

Kwani mtoto akinunua gari mtu mzima mwenye umri kama baba yake asipande kwasababu yeye ni mtu mzima na kama vipi angenunua la kwake?

LEAVE A REPLY