Barakah The Prince azipiga dongo nyimbo za wasanii wenzake

0
17

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Barakah The Prince amezipiga dongo nyimbo mpya za wasanii wa Bongo Fleva zilizotoka hivi karibuni kutokuwa na ubora.

Msanii huyo ameonyesha kutofurahishwa na aina ya muziki uanonekana kutamba zaidi hapa bongo kwasasa na ameamua kuwatolea uvivu wasanii wenzake kwa kuandika kuwa aslimia kubwa ya wasanii wenzake wanafanya mziki wa makelele.

Barakah amedai kuwa kwa mujibu wa sikio lake, asilimia kubwa ya nyimbo zilizotoka zimetawaliwa na kelele na zimekosa mada huku wasanii wakizingatia mwenendo wa kinachozungumziwa zaidi ‘Trend’ kwenye nyimbo zao.

Kupitia akurasa wake wa Instagram ameandika” Leo nimejaribu Kupitia Baadhi Ya Nyimbo MPYA Zimetoka hivi Karibuni,Nimegundua Katika 85% Miziki Hiyo..Ni Kelele Nyingi,Miziki Iliyokosa Topic Yani Fujo Fujo Tu Bora Li trend,Bora Liendee,Yani Bora walevi waka Bang ..Twapaswa Kujitafakari Wanamuziki Wa Kizazi ichi cha nyoka”

Katika maelezo yaliyohisiwa kuwa ni ushauri juu ya muelekeo wa Sanaa hiyo ya muziki kwa baadhi ya wasanii kwa mujibu wake, Barakah aliongeza kuwa ni muda sasa wa wawanamuziki kujitafakari juu ya hilo.

LEAVE A REPLY