Barakah The Prince amaliza tofauti zake na Alikiba

0
39

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Barakah The Prince amefunguka na kusema kuwa amewasamehe aliyekuwa meneja wake, Seven Mosha pamoja na Alikiba kwani hawawezi kumlipa kwa dhuluma walizomfanyia.

Barakah The Prince amesema ameamua kusamehe, kusahau na kutofuatilia yaliyotokea japo anaamini waajiri wake wa zamani bado wana kinyongo naye.

Amesema kuwa “Naomba leo tufunge mjadala wa Alikiba na Seven Mosha, sina noma na mtu yeyote labda wao ndiyo wana noma na mimi nimezika na nimefukia muda mrefu sana maana hawawezi kuwa na pesa ya kunilipa kwenye kipaji changu kama nikiamua kufuatilia kutokana na dhuluma na vitu vyote walionifanyia, nitakuwa namuonea tu”.

Barakah The Prince alisainiwa Rockstar4000 mwaka 2016 chini ya Mkurugenzi na meneja lebo hiyo Seven Mosha na msanii Alikiba ambaye ni mshirika wa kampuni hiyo kwa upande Afrika Mashariki.

LEAVE A REPLY