Baraka The Prince kuja na ngoma mpya

0
507

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Barakah The Prince ametangaza kuachia wimbo wake wa kwanza ‘Nimekoma” kwa mwaka 2020.

Barakah The Prince amesema kuwa ni wimbo ambao ameutunga kwa hisia kali na unatoka leo, Ukiwa umeandaliwa na Producer, Dee Classic.

Pia Barakah The Prince ameeleza sababu za kukaa kimya kwenye muziki kwa takribani mwaka mmoja, Na kudai kuwa alikuwa chimbo akiandaa Album yake ya kwanza na mambo ya kifamilia.

“Nimerudi rasmi kwenye gemu baada ya kukaa kimya bila kutoa ngoma mwaka 2019 lakini sasa nimeamua kurudi rasmi kwa kuwa game inanihitaji”.

Pia Baraka amesema kuwa alijichimbia kuandaa kazi zenye viwango, Na naahidi ujio wangu wa ngoma ya ‘Nimekoma’ utakuwa ni mwanzo tu kwani nina ngoma kibao ambazo zitatoka mwaka huu, Na zitakuwa pia kwenye Album yangu ambazo zitatoka mwaka huu Mungu akipenda,” amesema Barakah.

Baraka aliyewahi kutamba na ngoma kama Acha Niende, amesema kuwa audio ya wimbo wa ‘Nimekoma’ inatoka leo Alhamisi na huku video yale itatoka wiki hii pia.

LEAVE A REPLY