Baraka The Prince ashauri kufungwa kwa kisiwa cha Mbudya

0
137

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Baraka The Prince ameishauri serikali kukifunga kisiwa cha Mbudya kwa muda mpaka pale kutakapo boreshwa na kuwekwa kwa huduma za msingi katika kisiwa icho.

Baraka amesema kuwa kisiwa icho kimekuwa kikiingiza pesa kwa sababu ya watu wengi wanaoenda huko hivyo uweoz wa kuweka maboresho unawezekana na kama haiwezekani basi ni bora kukifungwa kwanza.

Kisiwa hicho kimekuwa hatarishi kwa maisha ya binadamu na hata kupoteza maisha ya watu wengi sana kutokana na mazingira yake kuwa hatarishi kwa wanaokwenda maeneo hayo.

Wasaii wanazidi kuguswa na swala hilo kutokana na kuwa wamkuwa wakienda na kuona matukio ya vifo vya watu mara  nyingi  na hata hivi karibuni kupoteza producer Pancho Latino.

Malalamiko hayo yamekuwa yakitolewa na watu tofauti tofauti na sasa ni jukumu la serikali na uongzo wa kisiwa icho kurekebisha baadhi ya vitu vya muhimu ili kuokoa maisha ya watu.

LEAVE A REPLY