Baraka The Prince akanusha kuwa na bifu na Alikiba

0
87

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Barakah The Prince amesema kuwa hajawahi kuwa na tofauti yoyote na msanii mwenzake Alikiba bali watu tu ndio wanaeneza maneno kwenye mitandao ya kijamii.

Baraka The Prince amesema hayo baada ya kumtakia kheri ya siku ya kuzaliwa Alikiba wakati kukiwa na tetesi kuwa hawaelewani lakini kitu ambacho siyo kweli.

Barakah amesema kuwa hilo kila mtu anaweza kulichukuliwa kwa matazamo wake ila yeye hana tofauti na Alikiba kisa kuondoka RockStar4000.

Baraka The Prince amesema kuwa hajawahi kuwa na matatizo na Alikiba na hajawahi kufikiria kuwa na matatizo naye.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa maneno hayo yametokea baada ya kuondoka kwenye kampuni ya RockStars4000.

Baraka The Prince amesema kuwa kila mtu anaweza kuichukulia tofauti lakini yeye huwa anaishi bila kuangalia amemridhisha nani au kufanya kwa ajili ya nani kwa sababu anajua hayo ndio maisha yake na wapi anataka kufika.

LEAVE A REPLY