Baraka The Prince afunguka ma-Dj kuambiwa kuacha kupiga nyimbo zake

0
102

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Baraka The Prince amesema kuwa baadhi ya ma-Dj nchini waliambiwa wasicheze nyimbo zake.

Baraka The Prince amesema kuwa  taarifa zilikuwa zinamfikia kutokana anaishi na watu vizuri na si kama inavyokuwa ikienezwa.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa “Kuna baadhi ya Dj’s walikuwa wanaambiwa wasicheze nyimbo zangu, wengine mpaka hela wanapewa kwa ajili ya kutopiga, unakuta mpaka Dj anakufuata anakuambia unajua nimepewa mpaka hela nyimbo yako nisipige.

Pia amesema kuwa  “Kwa hiyo hicho ni kitu cha kushukuru ingekuwa watu hawanipendi nina matatizo na watu inavyokuwa ikienezwa sidhani kama hata kuna mtu angeweza kuthubutu kunifuata na kunipa taarifa kama hizo, it means napendwa na watu na tayari nina empire yangu” .

Lakini Barakah hajaweka wazi ni kina nani hasa walikuwa wanashinikiza nyimbo zake zisipigwe redioni

LEAVE A REPLY