Baraka The Prince afungua kesi dhidi ya meneja wa RockStar4000

0
235

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Barakah The Prince amesema kuwa amefungua kesi dhidi ya aliyekuwa meneja wake wa RockStar4000, Seven Mosha baada ya kudai kufanyiwa figisu vigisu kwenye mtandao wake wa Youtube.

Baraka amesema hayo baada ya akaunti yake ya Youtube kuchezewa mpaka kusababisha views wake kupungua kwenye akaunti yake hiyo.

Msanii huyo amesema kuwa anahisi kabisa wanaofanya mchezo huo ni meneja huyo Seven Mosha wa RockStar4000 na mfanyakazi wa MX Carter kwani ndiyo wanaojua password ya akaunti yake.

Baraka amesema kuwa watu hao wawili ndio anawashuku kufanya hivyo kwani wao ndio walikuwa na password za account zote mbili.

Baraka ameendelea kusema kuwa baada ya akaunti yake ya kwanza kuchezewa akaamua kufungua akaunti nyingine ya Youtube lakini bado imeendelea kuchezewa na kusababisha views wake kupungua.

Pia ameongeza kuwa suala hiyo tayari limeshafunguliwa kesi mahakamani. Barakah aliwahi kuwa chini ya usimamizi wa RockStar4000 na baadae kujitoa.

LEAVE A REPLY