Baraka akanusha kushuka kimuziki

0
46

Mwamuziki wa Bongo Fleva, Barakah The Prince ameibuka na kudai kuwa hajashuka kimuziki kama ambavyo imekuwa ikidaiwa kwenye Mitandao ya kijamii.

Barakah alikuwa amesiniwa chini ya staa wa Bongo fleva Ali Kiba Kupitia Label yake ya Rockstar 4000 lakini Barakah alijitoa kutokana na kutofautiana na uongozi Wake.

Baada ya kuachana na Label hiyo Barakah amekuwa hana hit song kama zamani na pia amedaiwa kuwa amefulia kimuziki pia kumaanisha hajapata wimbo uliosumbua redioni kwa miaka kadhaa sana.

Barakah amekataa Tetesi Za yeye Kufulia na kusema kuwa hakufulia bali aliamua kupumzika na kuwapa nafasi wasanii wengine.

Mwanamuziki huyo amefunguka na kusema kuwa hajashuka kimuziki lakini alikaa pembeni ili kuwapisha wasanii wengine wachanga waweze kuonekana.

Pia amesema kuwa hataki kukubaliana na usemi kuwa ameshuka bali amerudi rasmi na hata ukiangalia hapo nyuma ngoma alizokuwa anatoa alikuwa aendi kwenye media kama wanavyofanya wanamuziki wengine.

LEAVE A REPLY