Baraka akanusha kufulia

0
57

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Barakah The Prince amefunguka na kukanusha habari zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa mwanamuziki huyo amefulia baada ya maisha yake kushuka tofauti na hapo awali.

Baraka amesema kuwa habari hizo hazina ukweli wowote kabisa kwa kuwa akuwahi kuwa na maisha ya kihivyo mpaka kufikia kufirisika wakati yeye maisha yake ni ya kawaida.

Tetesi hizo zimezidi kupamba Moto sasa hivi kwa sababu Barakah ameonekana kukonda kupita maelezo hali iliyopelekea wengi kufikiria huenda ni kwa sababu ya maisha magumu.

Barakah amesema kuwa yeye hajawahi kuwa tajiri na hivyo kwasasa ndio ameanza kuitafuta hela yake kwa kuanza kufanya kazi zake mwenyewe huku akidai kuwa yeye sio msanii wa kuweka maisha yake hadharani.

Pia Baraka amefunguka na kusema kuwa yeye ni mmoja wa wasanii ambao awapendelei sana kuweka hadharani maisha yake binafsi tofauti na muziki.

LEAVE A REPLY