Baraka akamatwa kisa utapelo

0
91

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Barakah The Prince amekamatwa na polisi jijini Dar es Salaam baada ya kudaiwa kumtapeli mwanamke mmoja aliyemtaka kimapenzi.

Jana kuna video ilisambaa kwenye Mitandao ya kijamii iliyomuonyesha Barakah akiwa anabishana na maaskari ambao walikuwa wanamkamata na mara moja ilisemekana aliwekwa chini ya ulinzi na kupelekwa kituoni.

Stori za chini ya kapeti zinadai kuwa Barakah aliokuwa polisi Baada ya kudaiwa kufanya utapeli ambapo inadaiwa alimtapeli mdada mmoja kiasi Chan shilingi milioni tano kwa ahadi ya kumpa Penzi Lakini Baraka aliishia kuchukua pesa hiyo na kununua gari.

Ulipofika muda wa kumpa penzi mdada yule ambaye alikuwa amemzimikia msanii huyo alimpa taarifa kuwa yeye hawezi kuwa naye kimapenzi kwa kuwa yupo na Mpenzi wake Naj.

Taarifa hizo zilimvuruga mdada huyo ambaye alihisi ametapeliwa kwani aliishia kumuitia polisi ambao walimtia ndani.

LEAVE A REPLY