Balozi wa China azindua ujenzi wa ofisi za walimu wa shule ya sekondari ya Makumbusho

0
110

Balozi China nchini Tanzania, Wang Ke leo amezindua ujenzi wa ofisi ya walimu katika shule ya sekondari ya Makumbusho jijini Dar es Salaam.

Pia Balozi huyo ameahidi kujenga ofisi nyingine nne za walimu  za Mkoa wa Dar es Salaam ili kusaidia  kuinua kiwango cha elimu.

Balozi  huyo  amesema nchi yake itaendelea kusaidia Tanzania  katika shughuli za maendeleo hususani  kujenga ofisi  za walimu ili utoaji elimu bure kwa watoto wa Tanzania  uende sambamba na mazingira mazuri ya walimu.

Kwa upande wa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemshukuru balozi huyo kwa kuahidi kujenga ofisi nyingine katika mkoa wake.

Makonda amesema kuwa China  imekuwa msatari wa mbele kwa kuiwezesha  Tanzania katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo na kuahidi kuendelea kuipa ushirikiano nchi hiyo kwa shughuli mbalimbali.

 Pia Makonda amewataka wananchi wa mkoa huo kuwapuuza viongozi wa kisiasa wanawaobeza wafadhili wanapotaka kujenga ofisi za walimu kwenye mkoa wake kwani waalimu ni watumishi wa umma na hawahusiani na masuala ya kisiasa.

LEAVE A REPLY