Bale ameanza mazoezi baada ya kupona majeraha

0
252

Kiungo wa klabu ya Real Madrid, Gareth Bale ameanza mazoezi na timu hiyo baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yanamsumbua hapo awali.

Kupitia akaunti yake ya Twitter Bale ameposti picha ikimuonesha akifanya mazoezi na wachezaji wenzake wa Real Madrid kwenye uwanja wa mazoezi wa timu hiyo mwishoni mwa wiki.

Bale mwenye umri wa miaka 27 amekuwa nje ya uwanja toka mwezi Novemba mwaka jana baada ya kuumia enka kwenye mechi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Sporting Lisborn ya Ureno.

Kwa upande wa kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane amesema kuwa anatarajia Bale atacheza kwenye mechi ya marudiano ya klabu bingwa Ulaya dhidi ya Napoli Machi 7 mwaka huu.

Naye kocha wa timu yake ya Taifa ya Wales Chris Coleman tayari amemjumuisha kiungo huyo kwenye kikosi cha timu hiyo kinachijiandaa kucheza mechi ya kufuzu kombe la dunia dhidi ya Jamhuri ya Ireland Machi 20 mwaka huu.

LEAVE A REPLY