Balaa MC aweka rekodi Audiomack

0
140

Baada ya kufanya vizuri kwenye Radio na Tv, mwanamuziki wa Singeli, Balaa MC ameweka rekodi ya kufikisha wasikilizaji 145k kwenye mtandao wa kusikilizia muziki wa Audiomack.

Nakuja ni moja kati ya ngoma ya miondoko ya singeli ambayo imepata nafasi kubwa ya kupenya mtaani,kwahii inaaminisha muziki wa singeli unazidi Kupata nguvu kubwa na kukubalika mtaani.

Original ya ngoma ya nakuja ilitoka april 14 mwaka huu na baadaye october 17 msanii Marioo alishiriki kufanya remix ya ngoma hiyo.

Balaa Mc anaingia kwenye orodha ya wasanii waliochipukia na kufanya vizuri Kwa mwaka huu kwenye digital platform ikiwemo Boomplay.

Tokea itoke rasmi ngoma hiyo ina jumla ya wasikilizaji 155K, Audiomack 145k na YouTube akiwa Na Subscribers 8.5K kutokana na mapokeo yake.

LEAVE A REPLY