Bad Boy yaongoza kwa mauzo

0
49

Filamu mpya ya Bad Boys For Life imekamata namba 1 kwa mauzo na kuweka rekodi ndani ya Box Office ndani ya siku nne toka filamu iachiwe rasmi nchini Marekani.

Filamu hiyo imeuza kiasi cha ($68.1 million) ndani ya siku 4 ukijumuisha na mauzo ya ($59.2 million) ya siku tatu za kwanza kwa mujibu wa The Hollywood Reporter.

Rekodi imewekwa kwa kuwa filamu ya pili iliyofanya poa kwenye mauzo katika wikendi ya kumbukumbun ya Martin Luther King.

Kidunia Bad Boys For Life imefanikiwa kuingiza kiasi cha ($107.3 million) kwenye masoko 39 ya uuzaji wa filamu duniani baada ya kutoka mapema mwezi huu.

Filamu hiyo imeigizwa na wasanii maarufu nchini Marekani, Will Smith na Martin Lawrance ambao wameonesha uigizaji wa hali ya juu kwenye movie mpaka kupelekea kufanya vizuri kwa muda mfupi.

LEAVE A REPLY