Baby Madaha akiri kuteswa na skendo ya unga

0
135

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Baby Madaha amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake hakuna kitu kilichowahi kumuumiza kama skendo ya kutumia dawa za kulevya.

Baby Madaha ambaye pia ni muigizaji wa Bongo Movie amesema kuwa suala hilo lilimletea sana shida katika familia yake mpaka kupelekea kuanza kumtenga kutokana na suala hilo la matumizi ya madawa ya kulevya.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa suala hilo lilitokana na kushiriki kwenye filamu mbalimbali akiwa kama teja.

Baby Madaha amesema kuwa kutokana na kuigiza kama teja ndiyo ilisababisha watu wazushe kwamba alikuwa akitumia madawa ya kulevya jambo ambalo amelipinga vikali.

 Pia Baby amekiri kuwa skendo hiyo ilimtesa sana kiasi kwamba familia yake wakajua kweli anatumia unga mpaka kupelekea kupelekwa kupimwa hospitali na mama yake mdogo ndiyo ikaundulika kama hatumi madawa ya kulevya.

LEAVE A REPLY