Babu Tale adhamiria kurudisha penzi la Diamond na Zari

0
255

Siku za nyuma zilisambaa habari katika mitandao ya kijamii kuwa Zari The Boss Lady ameachana na Diamond Platnumz, hatimaye wawili hao uhenda wakarudiana baada ya Babu Tale kutua Afrika Kusini kwa ajili ya kusuruhisha tatizo hilo.

Babu Tale ambaye ni meneja wa Diamond Platnumz wiki iliyopita alitua pande za Afrika Kusini kwa ajili ya kusuruhisha tatizo lililopo katika ya Diamond na Mzazi mwenzake Zari The Boss Lady.

Kupitia akaunti ya yake Instagram Babu Tale amesema kuwa akiwa kama mtu anayeheshimiana na Zari hakuna kitakachoshindikana kumaliza mgogoro huo kwani ni jambo dogo sana kwake kumaliza tatizo hilo.

Swali lililopo midomoni mwa mashabiki wa mwanamuziki huyo ni je Babu Tale atarudi na jibu zuri kutoka kwa Zari nchini Afrika Kusini na atakuwa tayari kumsamehe mzazi mwenzake huyo ambaye ni staa mkubwa hapa Bongo.

Mbali na Babu Tale kutaka kurejea kwa penzi la wawili hao, lakini pia mama mzazi wa mwanamuziki huyo Mama Dangote ambaye muda mwingi amekuwa akiwasiliana na Zari ambapo hutumiwa picha za wajukuu zake na kuziposti katika mtandao wa kijamii.

Pia Dada wa Mwanamuziki huyo, Esma Platnumz nae anapenda kurudi kwa penzi la kaka yake pamoja na baby mama huyo Zari kutokana na kuposti picha za Zari katika akaunti yake ya Instagram.

Kurudi kwa penzi hilo kumechochewa na video mpya ya Diamond inayokwenda kwa jina la Iyena ambayo humo ndani inaonyesha Diamond akifunga ndoa na Zari.

LEAVE A REPLY