Babu Seya na Papii Kocha wakanusha kujihusisha na siasa

0
76

Wasanii wa muziki wa dansi nchini, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na Papii Kocha wamesema kuwa hawawezi kujihusisha na siasa baada ya kutoka jela.

Kauli za wasanii zimekuja baada ya kuulizwa swali na waandishi wa habari kuwa wataonekana kwenye majukwaa ya siasa.

Kwa upande wa Papii Kocha amesema kuwa katika maisha yao ya muziki na sanaa hawataki kusikia kitu kinaitwa siasa na kusema wao siyo wanasiasa bali ni wasanii wa muziki.

Babu Seya na mwanaye Papii Kocha wamesema hayo baada ya kusikia tetesi za watu wakiwahusisha na masuala ya siasa na vyama vya siasa na kudai kuwa wao si wanasiasa bali wao ni wasanii wa muziki.

Wasaii hao wiki iliyopita walifanya show katika ukumbi wa King Solomon jijini Dar es Salaam na kuja watu ukumbini hapo.

LEAVE A REPLY