Baba mzazi wa Alikiba afariki dunia

0
180

Baba mzazi wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba, Mzee Salehe amefariki dunia katika hospitali ya taifa ya Muhimbili alipokuwa anatibiwa baada ya kuugua.

Abuu Kiba amesema mwili wa marehemu bado umehifadhiwa Muhimbili na msiba upo nyumbani kwao Kariakoo.

Pia Abdu amesema kuwa mazishi yatafanyika leo saa 10 jioni katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Mzee Kiba ambaye pia ni baba mzazi wa msanii Abdu Kiba na Zabibu Kiba amekua akiugua kwa muda sasa huku akiendelea kutibiwa.

LEAVE A REPLY