Baba Levo kuachia video ya Shusha akiwa na Diamond Platnumz

0
44

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Baba Levo amefunguka na kutangaza kuachia video rasmi ya wimbo wake mpya iliyogharimu zaidi ya milioni 24 za kitanzania aliyomshirikisha Diamond Platnumz.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Baba Levo alithibitisha kuwa leo ‘Jan. 26’ ataachia rasmi video ya wimbo wake Shusha ambao amefanya na mwanamuziki Diamond Platnumz.

Baba Levo alitangaza habari njema kuwa Diamond Platnumz amekubali kugharamia kiasi cha $10500 kwa video ya wimbo huo waliofanya wote.

Gharama alizokubali kulipa Diamond kwa ajili ya video ya wimbo huo ‘Shusha’ ambapo pia ameshirikishwa ni sawa na zaidi ya Milioni 24 za kitanzania.

LEAVE A REPLY