Baba Levo amshukuru Rayvanny

0
192

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Baba Levo amemwaga shukrani kwa msanii Rayvanny na kusema kuwa ndiye msanii aliyemrudisha kwenye gemu baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu.

Baba Levo amesema kuwa Rayvanny amejitoa sana kukamilisha na kuifanyia promo ngoma ya Zipo aliyomshirikisha Rayvanny na kwa kiasi kikubwa imelirudisha jina lake kwenye ramani.

Baba ameendelea kuwa kusema kuwa “Rayvanny ndiye anayenifanya mimi nitoke upya haswa kupitia wimbo wa Zipo kwa sababu aliniahidi atausukuma na amefanya hivyo kweli.

Pia ameendelea kusema Nimemchagua yeye kwa sababu naona tunapatana sana na ikiwezekana ninaweza nikafanya naye ngoma nyingine kama mbili tatu hivi,”.

Mwanamuziki huyo alitamba na wimbo wake ‘Kama Kawa’ aliomshirikisha Mwanamuziki nyota hapa nchini Juama Nature.

LEAVE A REPLY